Rwanda yafahamu nia ya Uingereza juu ya mpango wa uhamiaji – DW – 09.07.2024

Katika taarifa, msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo, amesema Rwanda inazingatia nia ya serikali ya Uingereza kusitisha Mkataba wa Ushirikiano wa Uhamiaji na Maendeleo ya Kiuchumi, uliopitishwa na mabunge ya nchi hizo mbili.

Soma pia:Serikali ya Starmer yaanza kazi kwa kufuta mpango wa uhamiaji wa mtangulizi wake Rishi Sunak

Taarifa hiyo pia imesema ushirikiano huo ulianzishwa na serikali ya Uingereza ili kushughulikia mgogoro wa uhamiaji usio wa kawaida unaoiathiri nchi hiyo na kwamba ni tatizo la Uingereza na sio Rwanda.

Rwanda yasema imetimiza upande wake wa makubaliano

Makolo ameongeza kuwa Rwanda imetimiza kikamilifu upande wake wa makubaliano, ikiwa ni pamoja na suala la fedha, na bado imejitolea kutafuta suluhu la mzozo wa uhamiajiduniani, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usalama na kutoa fursa kwa wakimbizi na wahamiaji wanaoingia nchini humo.

Wahamiaji wa Ethiopia washuka kutoka boti katika ufuo wa bahari wa Ras al-Ara, Lahj nchini Yemen mnamo Julai 26,2019
Wahamiaji wa EthiopiaPicha: Nariman El-Mofty/AP Images/picture alliance

Hii ni mara ya kwanza kwa mamlaka ya Rwanda kutoa maoni rasmi juu ya mipango ya serikali mpya ya Chama cha Labour cha Uingereza kufutilia mbali mpango huo ambao uliosababisha ukosoaji mkubwa kutoka kwa watetezi wa haki za binadamu walioutaja kuwa wa ukatili na unyama.

Soma pia:Waziri Mkuu Sunak ashinda mtihani wa uongozi kuhusu mpango wa Rwanda…kwa sasa

Haikubainika wazi kama mamlaka hiyo ya Rwanda ilikuwa inajibu ripoti za vyombo vya habari au ilikuwa imepewa taarifa rasmi ya mipango ya kusitisha makubaliano hayo.

Soma pia;UN yaitaka Uingereza kufirikia upya sheria yake ya uhamiaji

Siku ya Jumamosi, waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer, alitangaza kuwa mpango huo wa uhamiaji ulioanzishwa na serikali ya kihafidhina iliyoondolewa madarakani umefutiliwa mbali.

 

Related Posts