Sababu mbili ndizo zilizofanya timu ya wanawake ya Mchenga Queens ipoteze mchezo wake kwa pointi 72-34 dhidi ya DB Troncatti katika Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL).
Mchezo huo wa mzunguko wa pili kwa timu hizo ulifanyika katika wa Donbosco, Osterbay.
Sababu ya kwanza iliyoiua Mchenga Queens ilitokana na wachezaji kutokuwa makini katika pasi walizokuwa wanapasiana, hivi kuangukia kirahisi kwa wapinzani wao.
Hatua hiyo ilitokana na kukosa umakini kulikofanya DB Troncatti ichukue mpira kirahisi na kwenda kufunga.
Sababu ya pili ni kutokana na mfumo iliokuwa inautumia DB Troncatti wa kupeana pasi ndefu maarufu kama fast break.
Mfumo huo uliwachanganya wachezaji wa Mchenga Queens waliokuwa wazito kurudi nyuma kulinda goli lao, ambapo
katika mchezo huo DB Troncatti iliongoza katika robo zote nne kwa pointi 13-7, 16-11, 26-9, 17-17.
Katika mchezo huo, mchezaji Tumwagili Joshua wa DB Troncatti aliongoza kwa kufunga pointi 19 akifuatiwa na staa mwenzake, Jesca Lenga aliyefunga pointi 14.
Kwa upande wa Mchenga Queens alikuwa Fatma Yassoda aliyefunga pointi 14, akifuatiwa na Aziza Juma aliyetupia alama nane.
Katika mchezo mwingine uliochezwa uwanjani hapo Twalipo Queens iliifunga Kigamboni Queens kwa pointi 49-34.