TETESI ZA USAJILI BONGO: Lomalisa Mutambala kutimkia Linafoot

KLABU ya Linafoot ya Congo ipo kwenye mazungumzo na beki wa zamani wa Yanga, Joyce Lomalisa baada ya kumaliza mkataba na wananchi hao.

Mazungumzo baina ya Lomalisa na Linafoot bado yanaendelea na kama mambo yatakwenda sawa anaweza kujiunga nao ingawa awali alikuwa akihusishwa na klabu mbalimbali nchini ikiwemo Namungo na Simba na FC Lupopo ya kwao Congo.

Inaelezwa awali FC Lupopo ilikuwa ya kwanza kufanya mazungumzo na Lomalisa baada ya beki wa timu hiyo, Shadrack Boka kujiunga na Yanga kuchukua na nafasi yake.

Kama mkongomani huyo atasajiliwa Lupopo atakwenda kuziba pengo la Boka ambaye tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kukitumikia kikosi hicho.

Ndani ya misimu miwili aliyocheza Lomalisa amefanikiwa kuchukua mataji mawili ya Ligi Kuu Bara, Kombe la ASFC, Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kucheza robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Related Posts