Urusi yashambulia droni za Ukraine kwenye maeneo ya mipaka – DW – 09.07.2024

9 Julai 2024

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema mifumo yake ya ulinzi wa anga imeharibu droni 38 za Ukraine usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya mpakani ikiwemo Belgorod,Kursk,Voronezh,Rostov na Astrakhan.

https://p.dw.com/p/4i3Qu

Zana za kivita za Ukraine zikiwa katika eneo la Donetsk
Zana za kivita za Ukraine zikiwa katika eneo la DonetskPicha: Narciso Contreras/Anadolu/picture alliance

Gavana wa jimbo la Astrakhan Igor Babushkin amesema Ukraine ilianzisha jaribio la kufanya mashambulizi makubwa yanayolenga maeneo ya Urusi kwa kutumia droni.

Soma pia: Xi atoa wito kuzisaidia Urusi na Ukraine kufanya mazungumzo

Taarifa zinasema kwamba pande zote mbili zimetumia droni ikiwemo ndege  zenye uwezo wa kuripuka zenyewe katika eneo la umbali wa mamia ya kilomita.
 

Related Posts