KLABU ya Yanga imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji, Aziz Andambwile kutoka Singida Fountain Gates kwa mkataba wa miaka miwili.
Kiungo huyo amejiunga na Yanga kuongeza nguvu eneo la kiungo cha ukabaji ambapo anaungana na Khalid Aucho na Jonas Mkude.
Usajili wa kiungo huyo unamaanisha kwamba anakwenda kuchukua nafasi ya Zawadi Mauya ambaye hivi karibuni aliondoka baada ya mkataba wake kumalizika akiwa ameitumikia timu hiyo kwa miaka minne kuanzia 2020 hadi 2024.
Andambwile anakuwa mchezaji wa tano mpya kutambulishwa ndani ya Yanga kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa baada ya Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka na Khomeiny Aboubakar.