Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Kimataifa la Sauti ya Nigeria (VON), Jibrin Baba Ndace ametembelea Studio za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kujionea maboresho ya kisasa ya studio hizo.
Jibrin amepokelewa na mwenyeji wake, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba Chacha na kumtembeza katika studio hizo za kisasa zilizopo Barabara ya Nyerere na Mikocheni mkoani Dar es Salaam.
Jibrin amesema VON itaendelea kushirikiana na TBC katika ngazi mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu pamoja na watendaji na kwamba VON imeanza kufanya hivyo.
Cc:TBC