Ifahamu Meli ya Hospitali ya Ark Peach inayotarajiwa nchini

Dar es Salaam. Meli ya Hospitali ya Ark Peace inatarajia kutia nanga katika Bandari ya Dar es salaam mwanzoni mwa wiki ijayo kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu wa watu wenye matatizo ya afya na uchunguzi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ubalozi wa China nchini Tanzania meli hiyo iliyobeba madaktari zaidi ya 100 waliobobea katika magonjwa mbalimbali itawasili nchini Julai 16, 2024 na itakaa hadi Julai 23, 2024 na matibabu yote yatatolewa bure.

Mali hiyo iliundwa nchini China, ilizinduliwa rasmi Desemba 2008 na kupewa namba 866. Urefu wake ni mita 178, upana wa mita 24 na urefu wa mita 35.5.

Uwezo wake wa kuhimili upepo ni Force 12 na kasi ya juu ya noti 20. Ndani yake helikopta moja ya uokoaji inapatikana ndani.

Meli ina maeneo matano ya matibabu yakiwamo yale maalumu kwa ajili ya majeruhi, triage, wagonjwa wa nje, kulazwa na uokoaji na vyumba vinane vya upasuaji.

Ark Peace ina vifaa vya matibabu kama vile CT Skana, mifumo ya DR, uchunguzi wa Color Doppler, gastroskopu, vichanganuzi vya biokemikali, vifaa vya kusaidia na vingine vingi zaidi ya seti 2,030 na vifaa vya matibabu aina 250 tofauti.  

Tangu Ark Peace itengenezwe imeshatoa huduma za nje mara tisa (mwaka 2010, 2011, 2013, 2014, 2015, 2017, 2018, 2022 na 2023), imekwishatembelea nchi 46 katika bahari tatu na mabara sita, ilitoa huduma za matibabu kwa watu 290,000, kwa hiyo, inasifika kama Meli ya Uhai.

Mali hiyo ina zaidi ya wafanyakazi 100  wa matibabu. Miongoni mwao, asilimia 74 ni wataalamu wa ngazi ya kati hadi wa juu na asilimia 67 kati yao wamewahi kufanya shughuli maalumu za kimatibabu.

Miongoni mwa madaktari bingwa waliopo katika meli hiyo ni wale mifumo ya fahamu, afya ya uzazi, mifupa, meno na magonjwa ya jumla.

Wagonjwa wanaohitaji upasuaji watapata huduma hiyo endapo matibabu yao yatakuwa ni yale yanayochukua chini ya siku saba.

Related Posts