Khan, Whyte wamjaza Tyson | Mwanaspoti

MABONDIA Amir Khan na Dillian Whyte wametoa mtazamo wa pambano la marudiano baina ya mabondia Tyson Fury na Oleksandr Usyk linalotarajiwa kufanyika Desemba, mwaka huu, Saudi Arabia.

Kahn anakiri ugumu wa Fury kumpiga Usyk, lakini kama atajiandaa vyema atalipa kisasi kwani ana uwezo wa kumpiga mpinzani wake huyo. Whyte kwa upande wake amemtaka Fury kutojiamini sana kushinda kiasi akashindwa kujiandaa kikamilifu kama ilivyokuwa pambano la kwanza, akitarajia bondia huyo alipize kisasi kwa pointi na sio kumpiga knockout ‘KO’.

Pambano hilo la uzito wa juu (heavyweight) litakuwa limetanguliwa na pambano la kuwania mkanda wa IBF, kati ya Daniel Dubois dhidi ya Anthony Joshua mwezi Septemba, na mshindi atasubiri mshindi wa pambano la marudiano kati ya Usyk na Fury ili kurudisha mataji manne ya uzito wa juu duniani aliyoshikilia Usyk baada ya kumchapa Fury.

Mara kadhaa Fury amekaririwa akisema haelewi alishindwaje kwa pointi za majaji dhidi ya Usyk kwani kila alipotazama marudiano ya pambano anaona alimzidi maradufu Usyk aliyekubali wazi kumvuruga kwenye raundi ya tisa aliyookolewa na ulingo.

Related Posts