Mjumbe wa Halmashauri Kuu (CCM) mkoa wa Songwe, Ombeni Nanyoro ametoa msaada wa tofali 10,000 na bando sita za bati kuchangia ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa chama hicho. Anaripoti Ibrahim Yassin, Sumbawanga…(endelea).
Nanyaro aliyekuwa mgeni rasmi jana kwenye kwenye Baraza la Umoja wa vijana (VCCM ) wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, ametoa msaada huo wenye thamani ya Sh milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo.
Alisema anawashukuru wanachama hao kwa kumwalika kushiriki mkutano huo ambao unatumika kubadilisha maisha ya mtumishi huyo.
Akipokea msaada huo, Katibu wa Jumuiya ya vijana (UVCCM ) wilayani Sumbawanga, John Mwakifuna, amemshukuru Nanyaro kwa msaada huo huku akisema fedha hizo ni aIama kubwa iliyopandwa kwenye Jumuiya hiyo.
“Mgeni rasmi fedha hizi zinatumika kununua bati na tofali leoleo na pindi ujenzi utakapokamilika nitakualika uje kuizindua na kuipa baraka kwa sababu hakika umeiheshimisha Jumuiya hii,” amesema Mwakifuna.