Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Uganda-Tanga wafikia asilimia 30

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema amesema mradi bomba la mafuta la EACOP kutoka Hoima nchini Uganda Hadi Chongoleani Tanga unaendelea na umefikia asilimia 30 ambapo kazi hiyo ni kutandika mabomba .

Mramba ameyamebainisha hayo katika banda la Shirika la Maendeleo Petroli Tanzania(TPDC) alipotembelea katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema Mradi huo hadi sasa tayari kilomita zaidi ya 600 za mabomba zimetandikwa chini ya ardhi

Utandikaji wa mabomba hayo yanaenda vizuri ila kwa sababu mabomba yapo chini hayaonekani yamefikiwa, kulingana na ratiba ya mradi na hivi ninavyozungumza ’amesema Mhandisi Mramba.

Amesema mpaka sasa mradi huo umeshafanyiwa usanifu,ulipaji fidia ambapo wamebaki watu wachache ambao wana mambo ya mirathi.

Katika hatua nyingine Mhandisi Mramba amesema Serikali inatarajia kuongeza vituo vya kujaza gesi asilia kwenye magari kutoka viwili hadi vituo zaidi ya 30 vilivyopo mkoani Dar es Salaam.

Amesema ifikapo mwaka 2025 vituo hivyo vitawawezesha wananchi kupata huduma hiyo kwa urahisi zaidi.

“Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu tutakuwa tumejenga vituo maeneo ya Muhimbili,Kibaha,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),Sinza ,Mwenge,Goba ,Mbezi Beach na Mbagala,‘amesema Mhandisi Mramba.

Amesema kulingana na utaratibu uliopo vituo hivyo vya kujaza gesi kwenye magari baadhi vitajengwa na TPDC huku vingine vikitarajiwa kujengwa na sekta binafsi.

Amesema TPDC imejiongeza pamoja na kujenga vituo kwa mfumo wa kawaida uliozoeleka pia wataleta magari ambayo yatauza gesi huku yanatembea.

Aidha amesema mpaka mwakani kutakuwa na magari mengi yanaegesha huku akitolea mfano kuwa siku fulani wakiamua kuegesha Mwananyamala itakaa hapo na wateja wa maeneo hayo wataendana magari yao ili wajaziwe gesi.

Aidha alitoa wito kwa TPDC kuhakikisha wanatanua wigo wa usambazaji wa gesi asilia kwa kushirikiana na sekta binafsi. Lengo ni kuhakikisha gesi asilia inawafikia Watanzania wengi zaidi kwa haraka.



 

Katibu Mkuu wa Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba akiwa katika Banda la TPDC wakati alipotembelea Banda la TPDC Kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Related Posts