MWENYEKITI WA BODI AIPONGEZA FCC KWA KAZI NZURI VITA DHIDI YA BIDHAA BANDIA

 

 

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tume ya Ushindani FCC akizungumza na Roberta Feruz Mkuu wa Mawasiliano FCC kushoto na kulia ni Josephat Mkizungo Meneja wa huduma za Sheria FCC wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya 48 ya biashara ya Kimataifa  yanayoendelea viwnaja wa Sabasaba jijini Dar es Salaam. 

…………….,

Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani FCC Dkt. Aggrey Kalimwage Mlimuka leo ametembelea katika banda la taasisi hiyo inayoshiriki katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam ambapo kampuni mbalimbali za ndani na nje ya nchi zinashiriki zikiwemo taasisi na mashirika ya serikali. 

Dkt. Mlimuka ameipongeza Tume ya Ushindani FCC kwa kazi nzuri inayofanya kuhakikisha Tanzania inaondokana ama kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la bidhaa bandia nchini. 

Amempongeza Mkurugenzi Mkuu Bw. William Erio na Menejimenti ya FCC pamoja na wafanyakazi wote kwa kuhakikisha kazi inafanyika  kwa mafanikio  na kujituma katika ili kutekeleza kwa ufanisi majukumu yao. 

Kazi ya FCC ni pamoja na kulinda na kurahisisha ushindani wa kibiashara, kumlinda mlaji, kupokea na kusikiliza malalamiko ya wafanyabiashara dhidi ya vitendo vinavyokiuka sheria za ushindani na kudhibiti bidhaa bandia zisiingie, zisipitishwe na kuuzwa ndani ya mipaka ya Tanzania.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tume ya Ushindani FCC akizungum na  Josephat Mkizungo Meneja wa huduma za Sheria FCC wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya 48 ya biashara ya Kimataifa  yanayoendelea viwnaja wa Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tume ya Ushindani FCC akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea  banda hilo kwenye maonesho ya 48 ya biashara ya Kimataifa. 

Related Posts