Na Mwandishi wetu
WANANCHI Nchini wamekuwa na malalamiko mbalimbali kuhusiana na ubovu wa barabara.
Kutokana na hali hiyo Serikali pamoja na Taasisi mbalimbali zimekuwa zikijitokeza katika kufanya marekebisho ya barabara hizo.
Hivi karibuni Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Injinia Rogatus Mativila, alifanya ziara na kukagua barabara Mkoani Pwani.
Mkuu huyo alijionea barabara ambazo zinatakiwa kufanyiwa marekebisho na kutoa maamuzi huku akiwataka watendaji kufanya kazi kwa bidii.
mara baada ya kutembelea katika maeneo mbalimbali ambako barabara zinatengeneza akianzia Utete.
Alisema kuwa Serikali imejipanga vizuri katika kuhakikisha inafanya maboresho mazuri na ya kudumu katika Barabara zake kwa kuzifanyia matengenezo.
“Lakini Pia pamoja na kuziwekea lami katika Mkoa wa Mpwani hivyo kuwataka wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha barabara hizo zinajengwa kwa viwango vilivyowekwa kwa manufaa ya wananchi.
“Hapa Utete ambapo naona ujenzi unaendelea vizuri na tumesisitiza barabara ijengwe kwa ubora na kumalizika kwa wakati kwa manufaa ya wananchi lakini pia ipo ya kilometa 32 ambayo inachanganywa udongo na kemiko na hii inakaa muda mrefu,” alisema Naibu Injinia Mativila na kuongeza;
“Lakini hatukuishia hapo katika kuhakikisha Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatimiza mahitaji yake kwa wananchi, tumekuja hapa Muhoro, kutembelea daraja linalounganisha kwa kilomita 32 na hili usawa wake utakuwa mkubwa kwenda juu ili maji maji au mafuriko yasivuke kwenda maeneo mengine kwani tunatarajia kuwekwe tuta moja kwenda juu,”.
Alisema kuwa tayari mkandarasi amepewa maelekezo kuwa wanataka daraja lenye ubora ambalo hata baada ya kumalizika litakaa muda mredu sana bila kuleta tatizo lolote.
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini- Tanzania (TARURA) Injinia Leopard
Runji Pwani, alishukuru kwa ujio wa kiongozi huyo na kusema kuwa anaamini lengo kuu la Serikali katika kutatua kero za wananchi linatimia kwani serikali imekuwa ikiweka nguvu kubwa kwa katika kuhakikisha inatatua kero za wananchi wake katika kuwaletea maendeleo.
Alisema kuwa daraja la Muhoro ambalo awali lilijaa maji ya kutisha hivi sasa limepata ufumbuzi wa kina kwani wanaamini baada ya matengenezo hayo kuisha basi wananchi wataendelea kuishi kwa amani huku wakiendelea kutumia barabara zao bila matatizo na kwa muda mrefu.
“Tunaipongeza sana Serikali yetu kupitia Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani anafanya kazi mzuri, anaweka jitihada kubwa katika kuhakikisha wananchi wake wanapata maendeleo makubwa katika nyanja tofauti tofauti kwa ajili ya maendeleo wa Watanzania wote,” alisema Injinia Runji, na kuongeza;
“Lakini pia ni shukrani zetu za pekee kwa Naibu katibu mkuu kututembelea na kuona jitiada tunazoendelea nazo na pia tunamwakikishia kwamba maelekezo yote aliyotupatia tutayafanyia kazi bila kupepesa macho na kuhakikisha kila kitu kinaenda kilivyopangwa kwa wakati na kwa ubora kwa manufaa ya wananchi,”.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia ugeni na matembezi ya viongozi hao katika maeneo mbalimbali kwa ukaguzi wa kutekeleza miundombinu hiyo walipongeza sana.
Na kusema kuwa sasa wanaamini kinachofanyika hakina masihala badala yake serikali imejipanga kuwakwamua wananchi kwenye hali ngumu wanayokuwa wakikabiliana nayo ikiwemo mafuriko.
Zoezi la umaliziaji wa barabara linaendelea Pwani na wahusika wanaendelea kulisimamia vyema.
Mmoja wa wananchi aliyehojiwa na vyombo vya habari Mzee Athuman Salum Mkangama Mkazi wa Muhoro Kijiji cha Shela, alisema, ” baada ya mafuriko kila kitu kiliondoka ,” alisema.
Alisema kuwa hata majumba yalisombwa na maji na hivi sasa wanaanza upya na kilimo na kwamba mbali na hili pia wana njaa kwani viazi, mahindi, ndizi za kula na pia wanaanza upya kulima.
Aidha, alisema kuwa wakazi wa Muhoro hivi sasa wanachoiomba serikali ni msaada au Mashirika yoyote kuwapelekea mbegu za mpunga,mahindi Pamoja na Mihogo.
” Tuliwahi kuletewa msaada wa unga kilo 10 kila mtu ila ndio hamna tena ivyo tuwaumbe wadau na Serikali chini ya Mama Samia itus