Rais wa Kenya William Ruto amevunja baraza lake la mawaziri baada ya wiki kadhaa za maandamano yaliyoongozwa na kundi la vijana waliojulikana kwa jina la Gen Z. Kufuatia hatua hiyo, Naibu wa rais na Waziri Mkuu pekee ndio waliosalia.
“Baada ya kutafakari na kusikiliza kwa makini yale ambayo wananchi wa Kenya wamesema na baada ya tathmini ya kina ya utendaji wa Baraza langu la Mawaziri na mafanikio na changamoto zake, leo kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa nimeamua kuwatupilia mbali mara moja” Ameeleza Rais Ruto.
#KonceptTvUpdates