Captain Morgan Kunogesha Mbio za NBC Dodoma Marathon – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Serengeti Breweries Limited (SBL) inafuraha kutangaza kuwa chapa yake bora ya Captain Morgan, itakuwa mdhamini rasmi wa burudani na vinywaji katika Mbio za NBC Dodoma Marathon mwaka huu, 2024. Hii inakuja baada ya kusainiwa rasmi kwa Hati wa Makubaliano (MoU) baina ya SBL na National Bank of Commerce Limited (NBC), ambayo inarasimisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili huku Captain Morgan, ikisaidiwa na bidhaa nyingine za SBL, itatoa burudani na vinywaji kwa mwezi mzima mpaka mwishoni mwa wiki ya mbio hizo.

Mbio za NBC Dodoma, zitakazofanyika Julai 28, 2024, Dodoma, ni tukio la kipekee la kila mwaka la uwezeshaji ambalo huvutia washiriki kutoka maeneo yote Tanzania. Kupitia ushirikiano huu, Captain Morgan ina nafasi kubwa ya kuhakikisha tukio linakuwa la kipekee na kukumbukwa na washiriki wote. Hii inajumuisha burudani mbalimbali za starehe, kuonja bidhaa na mengine mengi ambayo yatafanyika Dar es Salaam na Dodoma, kuongeza ladha ya burudani kwa wote.

Udhamini wa Captain Morgan kwenye mbio hizi unaonesha ustahili wa chapa hiyo ya ushujaa na kufanya watu kuishi na kufurahia maisha, kama wengi watakaoshiriki mbio za Dodoma.

“Tunafuraha kushirikiana na benki ya NBC kwa ajili ya Mbio za Dodoma mwaka huu. Ushiriki wetu unadhihirisha kusudi letu la kusherehekea maisha kila siku, kila mahali, na ni chapa gani bora ya kuonesha hili zaidi ya Captain Morgan. Ingawa mbio hizi zinawavutia wakimbiaji wengi, kuna watazamaji wengine wengi wanaotafuta burudani – ambayo tunajitolea kutoa,” alisema Henry Esiaba, Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu wa Serengeti Breweries Limited (SBL).

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, alisema, “Tunafuraha kuwakaribisha Serengeti Breweries Limited (SBL), mshirika mashuhuri na mwenye mawazo ya kushabihiana nasi, kwa ajili ya shughuli hii adhimu na ya kipekee. Benki ya NBC, tunaamini kwa dhati kwamba juhudi za pamoja ni muhimu katika kukabiliana na changamoto zinazokabili jamii zetu. Kwa kutumia ujuzi na rasilimali mbalimbali, tunaweza kuongeza michango na kupanua wigo wetu. Inafurahisha kuwa SBL mbali na kuwa mshirika wa vinywaji pia inajumuika kwenye mawazo kama yetu na iko tayari kuleta msisimko na burudani tunapoungana kufikia lengo hili. Tunajivunia kuungana na washirika wote wenye mawazo yanayofanana ili kuimarisha jamii zetu kupitia juhudi za pamoja.”

SBL na NBC wamejidhatiti kufanya Mbio za NBC Dodoma 2024 kuwa tukio la kipekee na lisilosahaulika, likichanganya msisimko wa mbio na burudani za hali ya juu na uzoefu wa kusherehekea, hatimaye kuwaleta watu pamoja kwa roho ya furaha na umoja.

Washiriki wanakaribishwa kujisajili ili kushiriki hapa: [www.events.nbc.co.tz]

Related Posts

en English sw Swahili