TIMU ya DB Troncatti inaendelea kutesa katika ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BDL) upande wa wanawake, ikionyesha ubabe kwa kuifunga timu DB Lioness kwa pointi 72-55.
Katika mchezo huo, DB Troncatti iliongoza katika robo ya kwanza kwa pointi 19-12, 17-12, 22-16 na 14-15.
DB Troncatti ilimaliza mzunguko wa kwanza kwa kutopoteza mechi hata moja ikionyesha kupania kulitwaa taji la michuano hiyo.
Katika ligi ya mwaka jana, timu hiyo ilishika nafasi ya mwisho, jambo ambalo ni tofauti na mwaka huu ambao ni wazi inaonekana imedhamiria kuwaziba midomo walikuwa wanaibeza.
Hadi kufikia michezo 17 iliyocheza, DB Troncatti ilikuwa inaongoza kwa pointi 34, ikifuatiwa na Vijana Queens yenye pointi 30.