DROO YA LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA KUFANYIKA LEO – MWANAHARAKATI MZALENDO

Droo ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika itachezeshwa leo Cairo nchini Misri, kujua ni timu zipi zitacheza hatua ya awali ya michuano yote.

Yanga na Azam FC wataiwakilisha Tanzania, Ligi ya Mabingwa barani Afrika huku Simba na Coastal Union wataiwakilisha Tanzania, Kombe la Shirikisho ikiwa ni mara ya kwanza kwa wagosi wa kaya kushiriki michuano hiyo licha ya kuwahi kufanya vizuri miaka ya nyuma katika Ligi kuu.

Kwa mujibu wa mfumo wa CAF kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kupanga mechi za awali wana jumla ya makundi matatu, ambapo kuna timu tano ambazo hazitocheza hatua ya awali ( Preliminary) timu hizo ni Al Ahly ya Misri, Esperance ya Tunisia, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini , Petro Atretico ya Angola na TP Mazembe ya DR Congo.

Pia kuna timu nne (4) ambazo zinatambuliwa kama Highest Ranked yaani ziko na alama nyingi kwenye mfumo wa CAF ambazo timu hizo ni Yanga SC ya Tanzania, Pyramids ya Misri, Raja Casablanca ya Morocco na CR Belouzdad ya Algeria.

Ukichukua hizo timu tano za juu kisha ukijumlisha na hizo nne basi unaenda kupata jibu ya timu bora Afrika kwa mujibu wa CAF kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ‘Premier Club Competitions’, lakini bado Yanga ataanzia hatua za awali sambamba na hao wenzake watatu, ni timu tano tu hazitoanzia hatua za awali.

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho timu ambazo hazitaanzia hatua ya awali zipo 12 ambazo ni, Simba SC ya Tanzania, RS Berkane ya Morocco, FC Lupopo ya DR Congo, Stade Malien ya Mali na Enyimba FC ya Nigeria.

Nyingine ni pamoja na klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Zamalek SC ya Misri, USM Alger ya Algeria, AS Vita ya DR Congo, Shekukhune FC ya Zambia, EL Masry ya Misri pamoja na CS Sfaxien ya Tunisia.

#KonceptTvUpdates

Related Posts