Exim Bank yaendelea Kutoa Washindi wa Kampeni yake ya ‘Tap Tap Utoboe’ – MWANAHARAKATI MZALENDO

Exim Bank Tanzania imeendesha droo ya kwanza ya mwezi Julai katika kampeni yake ya ‘Tap Tap Utoboe’ ambayo wateja wa benki hiyo wanapata nafasi ya kujishindia fedha taslimu pamoja na zawadi zingine kama vile pikipiki, bajaji, na gari mpya aina ya Mazda CX-5.
Ili kushinda, mteja anatakiwa kufanya miamala yake ya kifedha kwa kutumia simu yake ya mkononi au mtandao anapokuwa anafanya manunuzi au kulipia huduma mbalimbali za kibenki. Katika droo hiyo ya nne, ambayo imefanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini
Dar es Salaam tarehe 10 mwezi huu, wamepatikana washindi 10 ambao kila mmoja anashindia fedha taslimu kiasi cha TZS 100,000/=.
Akitangaza washindi hao, Afisa wa Benki kutoka Idara ya huduma mbadala za kibenki na kidigitali, Thuweiba Bakary (kati kati), anasema, “Hii ni droo ya kwanza ya mwezi huu na washindi mbalimbali wamepatikana na hivyo kuweza kujishindia fedha taslimu ambapo mwishoni watapatikana washindi wa jumla ambao watajishindia piki, bajaji, na mshindi wa kwanza atashinda gari mpya.”
Kampeni ya Tap Tap Utoboe inalenga kuwahamasisha wateja wa Exim Bank Tanzania kujenga tabia ya kufanya miamala kidijitali na kisasa zaidi.

Hii ni sehemu ya benki hiyo kuunga mkono juhudi za serikali katika kuelekea kwenye uchumi wa kidijitali pamoja na maendeleo ya kiteknolojia. Thuweiba aliongeza kuwa benki hiyo imeridhishwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa wateja wake kufanya miamala kidijitali kufuatia kampeni hiyo.

#KonceptTvUpdates

Related Posts