MAHAKAMA ZISITOE DHAMANA KWA MAFISADI – MWANAHARAKATI MZALENDO

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni anasema ufisadi unaweza kumalizika kwa urahisi ikiwa Mahakama haitatoa dhamana kwa mafisadi.

Museveni ameyasema hayo wakati akihutubia Baraza la mawaziri katika Taasisi ya Uongozi ya Kyankwanzi, ambapo amesema msaada pekee unaohitajika kutoka kwa Mahakama sio dhamana kwa wale wanaotuhumiwa kwa mauaji, uhaini, ugaidi, ubakaji, unajisi, rushwa na wizi.

Na aliwakumbusha Polisi kuhakikisha wanaoiba katika Kampuni binafsi au Serikali, wawajibishwe kikamilifu ikiwa ni pamoja na kulipa fedha walizoiba pamoja na kifungwa.

Related Posts

en English sw Swahili