PURA yaweka mikakati ya kuongeza wawekezaji

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Khalfan Khalfan amesema kuwa PURA itahakikisha inaongeza wawekezaji kwenye maeneo ambayo yako wazi ili kuongeza matumizi ya gesi asilia kwa viwandani na majumbani .

Gesi asilia nyingi nchini hivyo kazi iliyopo ni kuendelea kushawishi wawekezaji katika kuja kuwekeza katika eneo hilo.

Serikali ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji na kazi kaifanya katika kuitangaza nchi katika mataifa mbalimbali juu ya kufanya uwekezaji nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara Kimataifa (DITF) Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Amesema PURA ina majukumu mawili makubwa nchini ya kusimamia na kudhibiti shughuli za Mkondo wa Juu wa Petroli.

Khalfan amesema kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana wawekezaji wa kutosha hivyo PURA itahakikisha inaongeza wawekezaji hao katika maeneo ambayo yapo wazi ikiwa ni kutumia majukwaa mbalimbali ya kuitangaza maeneo hayo kuwekezwa.

Amesema jukumu lingine la PURA ni kumshauri Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Petroli juu ya mambo yanayohusu mkondo wa juu wa Petroli nchini.

“PURA tunajukumu la kusimamia shughuli zote za mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika kwa ajili ya soko la nje ya nchi.”amesema Khalfan

Amesema mafanikio yaliyopatikana kwenye gesi asilia kuwa ni pamoja na kuchangia kwa wastani wa asilimia 50 ya Umeme unaozalishwa nchini, kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani, majumbani pamoja na matumizi ya gesi kwenye magari.

Khalfan Amesema watanzania zaidi ya 1,428 wamepata ajira za kudumu na za muda katika miradi ya ufatiliaji wa uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini hivyo imepunguza changamoto ya ajira kwa vijana.

“Kuanzishwa Kwa kazidata ya watoa huduma wa Kitanzania ambapo Kampuni za watu zaidi ya watu 2000 wamesajiliwa na huku kuongeza sh. Billioni 173 zimeokolewa kupitia kaguzi za mikataba ya uzalishaji na ugawaji wa mapato

Amezumgumzia maonesho haya kwa kusema awali yalikuwa kama gulio lakini kwa sasa yameboreshwa na kuwa na hadhi na kufurahiwa kwa wananchi katika kupata huduma.

Ameipongeza Tantrade kwa kusimamia na kuyawezesha maonesho haya na kuwa na hadhi ya Kimataifa “.amesema

Hata hivyo amewataka wawekezaji wenye uwezo kuwekeza kwa kuwa Tanzania ni sehemu salama pa biashara na uwekezaji.

Picha mbalimbali za Mwenyekiti wa Bodi wa PURA Khalfan Khalfan akiwa katika Banda la PURA kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Related Posts