Rais Samia ateua, amwapisha bosi mpya Usalama wa Taifa

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Suleiman Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).

Mombo anachukua nafasi ya Balozi Ali Idi Siwa ambaye amestaafu.

Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mululi Majula Mahendeka kupitia taarifa iliyosainiwa na Sharifa Nyanga, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu leo Alhamisi Julai 11, 2024. Mombo tayari ameapishwa na Rais.

Kabla ya uteuzi huo, Mombo alikuwa Ofisa Mwandamizi Ofisi ya Rais Ikulu.

Mombo anakuwa mkurugenzi mkuu wa nne kushika wadhifa huo, tangu Rais Samia alipoapishwa kushika madaraka hayo Machi 19, 2021.

Alipoingia madarakani Rais Samia, aliyekuwa na wadhifa huo ni Diwani Athumani aliyeteuliwa na hayati Dk John Magufuli. Diwani alishika washifa huo hadi Januari, 2023.

Rais Samia Januari 3, 2023 alimteua Said Massoro kushika wadhifa huo hadi Agosti, 2023 aliondolewa na Rais Samia kufanya uteuzi mwingine katika nafasi hiyo, akimteua Balozi Ali Idi Siwa katika nafasi hiyo.

Mabosi wa TISS tangu uhuru

1. Emilio Mzena (1961 hadi 1975)

2. Dk Lawrence Gama (1975-1978)

3. Dk Hassy Kitine (1978-1980).

4. Balozi Augustine Mahiga (1980-1983)

5. Luteni Jenerali Imran Kombe (1983-1995)

6. Apson Mwang’onda (1995-2005)

7. Othman Rashid (2005-2016)

8. Dk Modestus Kipilimba (2016-2019)

9. Diwani Athumani (2019 -2023)

10. Said Hussein Massoro (Januari – Agosti 2023)

11. Balozi Ali Idi Siwa (2023 – Julai 2024)

12. Suleiman Mombo (Julai 11, 2024 na kuendelea).

Related Posts