RC MAKONDA AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI ZA USALAMA MKOA WA ARUSHA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Na Mwandishi Wetu;

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda @baba_keagan amekutana na kuzungumza na Wakuu wa vyombo vya Usalama Mkoa wa Arusha, kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa huo mapema leo Julai 11, 2024.

Katika kikao hicho, Mhe.Makonda ameweka wazi kuwa lengo la kikao kazi hicho, ni kuwakutanisha wakuu wa vyombo hivyo vya usalama kufahamiana kwa zaidi na kujenga uelewa wa pamoja, na kuwa na mkakati wa pamoja kwa lengo la kusimamia usalama wa mali na raia wa mkoa huo kwa kuzingatia vigezo vinavyotegemeana kwa taasisi hizo.

Amesema kuwa, kikao hicho kimuwezeshe kila mmoja kwa nafasi na Taasisi yake, tufikiri kwa pamoja namna tunavyoweza kushikamana, ili kuhakikisha usalama wa mkoa katika kuhakikisha usalama wa wananchi na wageni wa ndani na nje ya nchi hususani watalii wanaoingia nchini kupitia mkoani Arusha.

“Licha ya kuwa kila raia ni mlizi lakini vyombo vya usalama vinalo jukumu kubwa la kuweka mazingira rafiki ya kuwezesha shughuli za kiuchumi hususani katika sekta ya utalii, zinafanyika kwa amani na utulivu ikiwa usalama utakuwa ni wa uhakika, leo tuweke mkakati wa kufanya kazi kama timu kwa kila Taasisi inatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana” Amesema Mhe. Makonda.

Amesema kuwa, mgeni yeyote anapopokelewa kwenye mipaka ya mkoa wa Arusha, Taasisi zote zinazohusika zihakikishe mgeni amekidhi vigezo, ili anapoanza kutembea ndani ya mkoa asisumbuliwe tena, awe huru kufanya shughuli zilizomleta Arusha kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za mgeni kuwepo nchini.

Aidha ameeleza umuhimu kufanya kazi na wanahabari wa mkoa wa Arusha, ili wawe na taarifa sahihi za shughuli zinazofanywa na Taasisi za usalama pamoja na kazi zinazoendelea, ili kuwa na uelewa wa pamoja na kuweza kutoa taarifa sahihi kutoka vyanzo sahihi kwa wananchi ili kupunguza kasi ya kuondoa taarifa za upotoshaji zinasababisha taaruki ambazo sio za msingi.

#KonceptTvUpdates

Inaweza kuwa picha ya Watu 4 na jukwaa
Inaweza kuwa picha ya Watu 6 na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 2

Related Posts