SAKHO APEWA ‘THANK YOU’ UFARANSA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Klabu ya Quevilly-Rouen Métropole (QRM) imevunja mkataba na winga wa zamani wa Simba SC, Pape Sakho kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Klabu hiyo ya Ligue 2 ya Ufaransa ilitangaza leo Alhamisi kufikia makubaliano na winga huyo kwa makubaliano ya pande zote, kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii

“Kwa makubaliano ya pande zote na QRM, winga wetu, anaondoka kwenye klabu. Tunamshukuru kwa nguvu zote alizotuletea, pamoja na ushiriki wake na faida” sehemu ya taarifa ya klabu hiyo.

Nyota huyo wa Senegal alijiunga na klabu QRM, Julai mwaka 2023 kwa mkataba wa miaka mitatu lakini amekuwa na mwenendo usioridhisha, alicheza mechi tatu tu msimu uliopita hakufunga bao wala kutoa assist.

#KonceptTvUpdatesImage

 

Related Posts