Na Mwandishi Wetu.
TangaBaada ya kushika nafasi ya pili kwa usafi kitaifa kwa upande wa shule za Sekondari za Shule ya Istiqaama ya Jijini Tanga imepania kuongoza kitaifa katika mashindano yajayo ya Afya wa Mazingira kundi la shule za Sekondari Tanzania Bara.
Katika masjindano yaliyofanyika mwaka huu Kibaha Pwani shule hiyo ilishika nafasi ya pili, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Dk. Philip Mpango alizindua mashindano hayo.
Mashindano ya mapema mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu ‘Mtu ni afya ‘yalifanyika Kibaha Mkoa wa Pwani kwa mara ya 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1973.Dk Mpango alisisitiza umuhimu wa kutunza Mazingira na kuendelea kuzingatia kanuni za afya, makamu wa Rais alizipongeza taasisi ambazo zimefanya vizuri katika swala la afya na usafi wa mazingira ambao kwenye kundi la shuleMwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mohamed Hamad Mohamed anasema kwa msimu ujao watafanya vizuri zaidi na kwamba lengo ni kuongoza kitaifa .
“Kwa upande wetu usihindi huu ni chachu ya kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.Pia Mwaka huu Shule hiyo ilishiriki kataka halfa ya Walimu na wanafunzi Bora wa Kemia , Fizikia na Baiolojia iliyoandaliwa na Mkemia Mkuu wa Serikali Jijini Dar es Salaam.
Mwalimu wa Kemia wa Shule ya Istiqaama ya Jijini Tanga Said Mdee (Kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.John Jingu katikati na Mkuu wa Shule ya Istiqaama Mohamed Hamad (wa tatu Kushoto) wakifurahia jambo kwenye hafla ya waalimu na wanafunzi bora wa Masomo ya Sayansi iliyoandaliwa na Mkemia Mkuu wa Serikali.