TIMU ya kikapu ya Veta ilidhihirisha ubora wake baada ya kuifunga timu ya B4 Mwadui kwa pointi 45-39, katika ligi ya kikapu mkoa wa Shinyanga iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mwadui
Kamishina wa ufundi na mashindano wa mkoa huo, George Simba aliliambia Mwanaspoti kwamba, ameridhishwa na ushindani ulioonyeshwa na timu zote mbili katika mchezo huo uliokuwa mzuri na wa kupendeza.
Akizungumzia kuhusiana na viwango vya uchezaji wa timu zinazoshiriki ligi hiyo, alisema vimeongezeka sana tofauti na ligi zilizopita.
Akizidi kuongea, alisema: “Kuongezeka huko kunatokana na mafanikio ya mkoa huu katika mchezo wa kikapu.”
Timu zinazoshiriki ligi hiyo ni Kahama Sixers, B4 Mwadui, Risasi na Veta.