ALIYEKUWA KATIBU WA CCM AHAMIA CUF – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amempokea aliyewahi kuwa Katibu msaidizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Othman Dunga.

 

Profesa Lipumba amemkaribisha leo Julai 13, 2024 wilayani Kondoa akiwa kwenye mkutano wa hadhara uliojumuisha viongozi wote wa kitaifa wa chama hicho.

 

Amevitaka vyama vya siasa wilayani hapo kufanya siasa safi kama falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan inavyotaka, kwani baadhi ya vyama vimeonekana kukosa haki pindi wanapoandaa mikutano yao.

 

Dunga hadi anakihama CCM, alikuwa ofisa mwandamizi katika idara ya siasa na uhusiano wa kimataifa.

Related Posts