Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2024, leo Jumamosi Julai 13, 2024 katika ofisi za Baraza hilo Zanzibar.
Jumla ya watahiniwa 113,504 walifanya mtihani wa kidato cha sita, mwaka huu ambapo ulifanyika kwenye jumla ya shule 931 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 258.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Said Mohamed amesema ufaulu kwa ujumla mwaka huu umepanda kwa asilimia 0.26 ukilinganisha na mwaka uliopita.
Aidha, amesema matokeo kwa masomo yote ufaulu wake upo zaidi ya asilimia 90.