Mshaambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Moses Phiri ameaga rasmi na kuthibitisha kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Phiri ameandika “Leo ndio siku ya mwisho mimi kuwa mchezaji wa Simba, shukrani zote ziwaendee wachezaji nilioshirikiana nao, viongozi wa Simba na Rais Mo Dewji kwa kunifanya kuwa sehemu ya historia ya Simba.
Mwisho kwa mashabiki wote wa Simba ,nawapenda sana asanteni kwa upendo na ushirikiano mlionipa, daima mtabaki moyoni mwangu, tutakutana tena mjini hapo bongo nikija kufanya biashara”
Simba imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kiungo mshambuliaji ambaye alikuwa katika klabu ya Power Dynamos kwa mkopo. Mkataba wa nyota huyo ulikuwa unamalizika mwaka 2025.
#KonceptTvUpdates