Teknolojia inavyorahisisha maisha: Leading East Africa Limited yaleta suluhisho la maji safi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kadri teknolojia inavyozidi kukua, maisha yanakuwa rahisi zaidi. Sasa, hakuna ugumu tena wa kusafisha maji ya kunywa au matumizi mengine kwa kuyasubiri kwa muda mrefu. Mashine za kisasa zinazoweza kukurahisishia kazi hiyo ndani ya muda mfupi zimekuwa suluhisho bora, na maji yako yanakuwa safi kwa matumizi.

Suluhisho hili linapatikana kupitia kampuni mashuhuri ya Leading East Africa Limited, inayojihusisha na uuzaji wa mashine za kuchuja maji na bidhaa nyingine kama samani za ndani na ofisi. Kampuni hii ina makao makuu yake Mbezi Africana, jijini Dar es Salaam.

Amina Nzulano, mwakilishi kutoka Leading East Africa Limited, alizungumza na Mtanzania Digital katika Maonyesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, na kuwahimiza Watanzania kuchangamkia mashine za kuchuja maji zenye uwezo wa kuondoa chumvi, magadi, na tope. Mashine hizi huchuja maji na kuyafanya kuwa salama kwa ajili ya kunywa na matumizi mengine, ikiwamo biashara.

Amina alisema kuwa kampuni yao inatoa mashine za kuchuja maji zenye saizi tofauti kulingana na mahitaji ya mteja. “Tuna mashine zinazofaa kwa viwanda na kampuni, zenye uwezo wa kuchuja maji lita 1,000 hadi 10,000 kwa saa moja,” alisema Amina.

Kwa matumizi ya nyumbani na shuleni, kampuni hiyo inatoa mashine zinazochuja lita 250 hadi 500 kwa saa. Aidha, Amina alibainisha kuwa kuna mashine ndogo inayochuja lita 11 kwa saa, ambayo inafaa kwa maji ya kisima au yale yanayosambazwa na mamlaka mbalimbali kama DAWASCO, kwa Dar es Salaam.

“Kuna watu ambao hawapendi maji yaliyochemshwa au kutiwa dawa, hivyo tunawakaribisha Watanzania kuchangamkia mashine hizi ili kupata uhakika wa maji safi na salama yasiyokuwa na harufu,” aliongeza.

Amina alieleza kuwa kumiliki mashine moja kati ya hizo hakuwezi kuhitaji kuchuja maji kwa njia ya kuchemsha au kutumia dawa za kusafisha maji. “Kabla ya kutengeneza mashine kwa mteja, kwanza lazima tupime aina ya maji na matumizi yake, kisha tutamshauri aina ya mashine inayofaa,” alisema.

“Kwa mtu, kampuni au taasisi kama shule kuwa na mashine hii ni faida kubwa, inapunguza usumbufu wa kupata maji safi na salama, hivyo tunawakaribisha ili wajidhihirishie kauli mbiu yetu ya Water Treatment Experts,” alisema Amina.

Pia, alieleza kuwa kampuni yao inatoa usaidizi wa matengenezo kwa wateja wanaonunua mashine hizo, hivyo kuwahakikishia huduma bora na rahisi kufikiwa. “Tuko tayari kusaidia katika matengenezo iwapo kutakuwa na uhitaji, kwani tunapatikana kirahisi na wataalamu wetu wapo muda wote. Kwa Watanzania wote wanaotaka uhakika wa maji safi na salama, Leading East Africa Limited ni suluhisho bora kwa mahitaji yao ya maji,” alisema Amina.

Kando na mashine za kuchuja maji, Leading East Africa Limited pia inajihusisha na uuzaji wa samani za ndani na ofisini kama sofa, matenki ya kuhifadhia maji, na sauna kwa ajili ya afya.

Kwa mawasiliano zaidi, wateja wanaweza kuwasiliana moja kwa moja kupitia namba 0653 331 117.

Related Posts