Aliyekuwa Mchezaji Nguli wa soka wa Afrika Kusini, Stanley ‘Screamer’ Tshabalala amefariki Dunia leo Julai 12, 2024 akiwa na umri wa miaka 75.
Itakumbukwa mnamo Machi mwaka huu, Tshabalala alipata majeraha baada ya kupigwa risasi alipovamiwa nyumbani na majambazi nyumbani kwake.
Tshabalala anakumbukwa kama gwiji wa soka na mwanzilishi wa klabu ya Kaizer Chiefs na mkufunzi wa klabu ya Mamelodi Sundowns.
“Familia ya Tshabalala na Orlando Pirates inatangaza kifo cha kusikitisha na kisichotarajiwa cha Stanley Tshabalala mchana wa leo hospitalini,” imeandikwa na klabu ya Kaizer Chiefs