HISPANIA MABINGWA EURO 2024, YAILAZA UINGEREZA 2-1

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

TIMU ya Taifa ya Hispania imefanikiwa kunyakua kombe la Euro 2024 mara baada ya kuichapa Uingereza mabao 2-1 katika fainali ambayo imepigwa kwenye dimba la Olympiastadion (Berlin) nchini Ujerumani.

Hispania walianza kupata bao kupitia kwa Nico Williams dakika ya 47 kipindi cha pili akipokea pasi kutoka kwa nyota Yamal.

Dakika ya 72, nyota anaekipiga kwenye klabu ya Chelsea Cole Palmer aliweza kuisawazishia timu yake kwa bao zuri akipokea pasi kutoka Jude Belligham.

Mikel Oyarzabal aliweza kufunga hesabu kwenye fainali hiyo kwa kupachika bao la pili na la ushindi akipokea pasi kutoka kwa Marc Cucurella dakika ya 86 ya mchezo.

Mchezaji bora wa mashindano tuzo imekwenda kwa nyota wa Machester City, Rodri.

Related Posts