KLABU ZA ROTARY NCHINI ZA PANDA MITI 1000 KUADHIMISHA MIAKA 100 YA ROTARY

KATIKA Kuadhimisha Miaka 100 ya Klabu za Rotary Duniani ,Klabu za Rotary Tanzania zimesherehekea miaka hiyo kwa Kupanda Miti ya Matunda Shule ya Msingi Mtakuja Kunduchi Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati huo Gavana wa Rotary Kanda (Tanzania na Uganda ) Agnes Batengas amesema Klabu za Rotary zimekuwa zikijikita saidia kusaidia Jamii hasa kuweka Mazingira rafiki kwa Wanafunzi kusoma kwa kuboresha Miundombinu ikiwemo Madawati na Kutoa Mafunzo ya Tehama kwa Walimu wa Shule za Msingi nchini.

Hata hivyo Batengas ameeleza kuwa Klabu za Rotary zimepanda Miti 1000 ya matunda mbalimbali ikiwemo Maembe,Mapera ,Mapapai ili iweze kuwanufaisha watoto hao kwa kuimarisha miili yao pamoja na kuleta vivuli shuleni hapo.

“Miti hii tumeipanda wakati sahihi kwani mvua ndio zimeanza hivyo tunategemea miti mingine itaanza kuleta matokeo baada ya mwaka 1 mingine miaka 2 itaanza kuleta matunda pamoja na vivuli na hewa safi.”

Hata hivyo ameeleza kuwa Klabu za Rotary zipo Afrika na zimeungana kuhakikisha zinapanda miti na pia zimeundwa kwa ajili ya Kusaidia Jamii za Kiafrika.

Pia amewataka Wananchi wote kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kupanda Miti mara kwa mara ili kuweka Mazingira mazuri ya Kivuli na matunda katika Maeneo yao.

Kwa Upande wake Rais wa Klabu ya Rotary Dar, Manisha Tanna amesema Klabu yao Wamepanda Miti 100 kwa hiyo kwa Lengo kuweka Mazingira mazuri lakini kwa ujumla klabu zote zimepanda Miti 1000 ya Matunda.

Pia ameongeza kuwa wamepanda miti ili kunusu Mazingira kwa majanga ya ukosefu wa mvua na mengineyo huku akiwasihi Wanafunzi hao wa Shule ya Mtakuja Kuhakikisha wanaitunza Miti hiyo shuleni hapo
 

Gavana wa Rotary Kanda Tanzania na Uganda Agnes Batengas akizungumza mara baada ya kukamilisha zoezi la upandaji Miti 1000 ya Matunda iliyopandwa na Klabu za Rotary nchini Tanzania katika Shule ya Msingi Mtakuja Kata ya Kunduchi wilaya ya  Kinondoni Jijini Dar es Salaam
 

Rais wa Klabu ya Rotary Dar Manisha Tanna akiwa pamoja na Wanachama wa Klabu hiyo wakiwa na miche ya Miti ya Matunda tayari kwa Kupanda katika eneo la Shule ya Msingi Mtakuja Kata ya Kunduchi wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam

Related Posts