Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa Taasisi zinazosimamia biashara na uwekezaji, Bara na Zanzibar kuhakikisha wanaondoa urasimu na kuwawezesha wafanyabiashara zaidi.
Rais Dkt.Mwinyi aliyasema hayo tarehe 13 Julai 2024, alipofunga Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya sabasaba, Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali zote mbili zina nia thabiti katika kuboresha mazingira ya biashara kwa kuelekeza taasisi za Serikali kusomana katika mifumo , kuondoa kodi na tozo kwenye maeneo ya kimkakati.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewahamasisha sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na wadau wa biashara kushiriki Maonesho makubwa ya Dunia ya Expo Osaka yanayotarajiwa kuanza tarehe 13 Aprili hadi 13 Oktoba 2025 kuvutia nchi zaidi ya 180 duniani ikiwemo Tanzania.