RAIS SAMIA AZINDUA MAKAO MAKUU YA POLISI KATAVI YALIYOGHARIMU BILIONI 1.4 – MWANAHARAKATI MZALENDO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 14, 2024, amezindua jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani humo. Ujenzi wa jengo hilo la kisasa umegharimu Shilingi Bilioni 1.4.

 

Kwenye hafla hiyo, Rais Samia alisisitiza umuhimu wa kuboresha miundombinu ya usalama nchini ili kuimarisha huduma kwa wananchi na kuleta maendeleo ya haraka.

 

Aidha, alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kudumisha amani na utulivu. Jengo hili jipya litatoa mazingira bora kwa maafisa wa polisi kutekeleza majukumu yao na kuboresha huduma kwa jamii.

Viongozi mbalimbali wa serikali na Jeshi la Polisi walihudhuria uzinduzi huo, wakitoa pongezi kwa hatua hii muhimu katika historia ya Mkoa wa Katavi.

Related Posts