SERIKALI INAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU – RAIS SAMIA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Katavi ambapo sasa barabara ya kutoka Tabora hadi Mpanda (km 352) ni ya kiwango cha lami.

 

Rais Dkt. Samia ameeleza hayo leo Julai 13, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Inyonga Wilayani Mlele wakati wa ziara yake mkoani Katavi.

 

“Wakati nimekuja kipindi cha kampeni kutoka Tabora kwenda Mpanda ilikuwa ni vumbi tupu lakini leo nimeteleza mpaka nimesinzia, Barabara ni nzuri na ni maendeleo makubwa sana, Niwapongeze sana”, amesema Dkt. Samia.

 

Dkt. Samia ameeleza miradi mingine inayoendelea kutekelezwa na Serikali katika Mkoa wa Katavi ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Kibaoni-Makutano ya Mlele (km 50), Vikonge – Luhafwe (km 25), Luhafwe – Mishamo (km 37) na Kagwira – Karema (km 110) kwa kiwango cha lami.

 

 

Related Posts