TAHADHARI ZA KUCHUKUA MJAMZITO KABLA YA KULA PAPAI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Mjamzito anaweza kula Papai katika kipindi chote cha Ujauzito bila kupata Madhara yoyote au Mimba yake kuharibika, endapo atafuata tahadhari husika kabla ya kula Tunda hili la Papai.

 

Kumekuwa na Usemi kwamba Mjamzito haruhusiwi kabisa kula Papai katika Kipindi cha Ujauzito, eti kwa sababu linaweza kusababisha Mimba kuharibika au Kujifungua Mtoto kabla ya wakati na kupelekea Mtoto kufariki au Changamoto nyinyine nyingi sana.

 

Ukweli ni kwamba Mjamzito anaweza kula Papai katika kipindi chote cha Ujauzito, Papai ni tunda muhimu sana kwa afya ya Mjamzito na Mtoto aliyeko Tumboni mwa Mjamzito, endapo Mjamzito unakosa Tunda hili basi unakosa Vitamini nyingi na Madini muhimu kwa afya ya Ujauzito wako.

 

TAHADHARI ZA KUCHUKUA MJAMZITO KABLA YA KULA PAPAI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO:

Mjamzito unapotumia Papai katika kipindi chako cha Ujauzito hususani Miezi mitatu ya Mwazoni au Miezi Mitatu ya Katikati ni vema kuzingatia Mambo haya Makuu mawili ambayo ni;

  1. Kula Papai liloiva vizuri, Mjamzito unapotaka kula Tunda hili la Papai unatakiwa kuhakikisha kuwa Papai limeiva vizuri, endapo halija iva vizuri ni vema usitumie katika kipindi chako cha Ujauzito.
  2. Kula Papai kiasi kidogo {Kula Vipande kadhaa tu}, Mjamzito unatakiwa kula Papai kwa kiasi kidogo tu au Vipande kadhaa na siyo Papai zima, ni vema kula kwa kiasi ili kuwa na afya bora katika kipindi chako cha Ujauzito.

KUMBUKA: Papai ambalo halijaiva huwa na Maji maji yenye rangi ya Maziwa ambayo huwa na kemikali iitwayo LATEX, kemikali hii huwa na vimeng’enyishi ambavyo huweza kuvunja vunja Protini katika Tishu za Mwanadamu au Mnyama ambavyo huitwa PAPAIN na CHYMOPAPAIN ambavyo wakati mwingine huweza kupelekea udhaifu wa kuta zinazomzunguka Mtoto aliyeko Tumboni mwa Mjamzito endapo Mjamzito alikula kwa wingi Papai lisiloiva au lenye LATEX nyingi katika kipingi cha Ujauzito.

Mojawapo ya Madhara ya Matumizi ya Papai bichi au Lenye LATEX nyingi ni kama;

  1. Mimba kuharibika kutokana na Mji wa Uzazi kukaza (Uterine Contractions) na Mimba kuharibika kabla ya wiki 28 (Miscarriage au Abortion).
  2. Kutokwa Damu katika kipindi cha Ujauzito, vimeng’enyishi vilivyomo kwenye Papai bichi mfano; Papai na Chymopapain huweza kupelekea kutokwa Damu kwa Mjamzito au Mimba kutishia kuharibika.
  3. Uchungu wa mapema kutokana na Mji wa Uzazi kukaza (Uterine Contractions) na kuanza kusukuma Mtoto nje kabla ya wakati wa Kujifungua.
  4. Chupa kupasuka kabla ya wakati, vimeng’enyishi vilivyomo kwenye Papai bichi mfano; Papain huweza kusababisha udhaifu wa kuta za chupa inayomzunguuka Mtoto na kupelekea Chupa kupasuka mapema.
  5. Kuvimba na inflamesheni ya eneo kuzunguka kingo za Kondo la nyuma la Mtoto lilipojishikiza kwenye Mji wa Uzazi na kupelekea changamoto kwa Mtoto aliyeko Tumboni na nk.

FAIDA YA MATUMIZI YA PAPAI KTK KIPINDI CHA UJAUZITO.

Endapo Mjamzito atatumia Papai lililoiva vizuri katika kipindi cha Ujauzito huweza kupata faida nyingi na muhimu kwa Ukuaji wa Mtoto aliyeko Tumboni na Mjamzito mwenyewe, faida hizo ni kama:

  1. Vitamini A, endapo Mjamzito atatumia Papai huweza kupata (Provitamin) au Carotene ambazo huweza kubadilishwa na Mwili kuwa Vitamini A ambazo ni muhimu katika Ukuaji wa Mtoto aliyeko Tumboni hususani Miezi Mitatu ya Mwishoni ya Ujauzito na kupunguza hali ya kutoona wakati wa giza kwa Mjamzito.
  1. Vitamini B, Papai huwa na Vitamini B za aina nyingi ikiwemo Vitamini B1,B2,B3, Vitamini B6 (Pridoxine) ambayo ni muhimu katika kupunguza kichefuchefu na kutapika kwa baadhi ya Wajawazito na Vitamini B9 (Folate au Folic Acid) ambayo husaidia kuongeza Damu kwa Mjamzito na kuzuia Mgongo au Ubongo wazi kwa Mtoto aliyeko Tumboni.
  2. Vitamini C, Huongeza kinga ya Mwili kwa Mjamzito na kupunguza utokwaji Damu kwenye fizi za Mjjamzito.
  3. Madini mfano Magnesium, Potassium, Zink na nk ambayo ni muhimu kwa Mjamzito.
  4. Nyuzi nyuzi, Papai huwa na nyuzi ambazo husaidia katika kupunguza hali ya choo kigumu (Constipation) kwa Mjamzito na katika kipindi cha Ujauzito.

Mjamzito unaweza kula Papai katika kipindi chako cha Ujauzito bila shida yoyote isipokuwa tuu, zingatia tahadhari kuu mbili Tajwa hapo juu ambazo ni Papai liwe limeiva na pia kula kwa kiasi kidogo tu, endapo Papai halijaiva ni vema kutotumia katika kipindi chote cha Ujauzito ili kuepuka Mimba kuharibika na nk.

 

Chanzo cha Makala Hii : Mama Afya Bora

Related Posts