TRUMP ASHAMBULIWA KWA RISASI – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Mgombea urais kupitia chama cha republican katika uchaguzi ujao nchi Marekani na Rais wa zamani Donard Trump ameshambuliwa kwa risasi kadhaa akiwa katika mkutano mjini Butler Pennsylvania.

 

Walinzi wake wamezunguka na kumuinua baada ya kuanguka chini huku akionekana kuvuja damu upande wa siko la kulia baada ya milio ya risasi kadhaa kusikika mkutanoni

 

Bado hajajulika nani alifyatua risasi, mashuhuda wanasema walisikia milio risasi kadhaa kutokea kwenye jengo pembeni na ulipokuwa ukutano na kisha kumuona Trump akianguka chini na kuzukwa na walinzi kwa mtindo wa kuatamia.

 

Bado haujajulikana kuwa damu zinazo tililika kutoka usoni ni sababu ya risasi au kuanguka chini ameondolewa akiwa mzima huku akiinua mkono kusalimia na kuaga akiwa anavuja damu usoni

 

Mtu mmoja amefariki baada ya kupigwa risasi zilizomkosa Trump.

 

Inadaiwa wadunguaji walikuwa wawili kutoka pande mbili tofauti na mmoja amekamatwa huku hali ya Trump ikiendelea kuimarika na amewashukuru walinzi kwa kazi nzuri.

Related Posts