YANGA inaendelea kushusha vyuma na safari hii imetua kwa beki wa kati raia wa Kenya, Anitha Adongo kwa ajili ya msimu ujao.
Hadi sasa Yanga Princess inayoshiriki Ligi ya Wanawake (WPL) inahusishwa kumalizana na wachezaji wanne wa kigeni akiwemo Danai Bhobho kutoka kwa watani zao, Simba Queens.
Akizungumza na Mwanaspoti, Rafiki wa karibu wa mchezaji huyo wa zamani wa Alliance Girls ya Mwanza alisema ni kweli Yanga ilimtafuta na kufanya mazungumzo naye kilichobani ni kusaini tu.
“Kwa sasa yupo Kenya kwenye mapumziko na Yanga walimtumia mkataba ausome na wakaelewana ingawa kulikuwa na ofa pia kutoka Fountain lakini mwenyewe hajaridhia huko kutokana na changamoto ya klbu hiyo,” alisema rafki wa mchezaji huyo na kuongeza
“Wanasubiri tu utaratibu kutoka kwa Yanga baada ya kuwarudishia majibu ya kuwa ameridhia kujiunga nao, atakuja kwenye tamasha la Yanga Day ndio atasaini mkataba.”
Anita msimu uliopita alikuwa nahodha wa Alliance Girls akiisaidia timu hiyo kubaki Ligi Kuu msimu ujao.