https://p.dw.com/p/4iJaq
Chama hicho kimesema kinataka kupata nafasi hiyo ili kuwa na nguvu bungeni licha ya kutokuwa na wingi mkubwa wa viti na kinashindwa kuunda serikali baada ya uchaguzi wa mapema wa bunge.
Wabunge watakuwa na jukumu Alhamisi la kumchaguwa spika,ambayo ni nafasi muhimu katika kipindi hiki ambacho rais Emmanuel Macron amedhoofika kisiasa na bunge likiwa na mgawanyiko kutoka na kutokuwepo chama au kundi lenye wingi wa kutosha wa kudhibiti mamlaka peke yake.