China na Urusi zafanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja – DW – 15.07.2024

Shirika la habari la China- Xinhua limetoa taarifa hiyo ikiwa ni siku chache baada ya washirika wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO kuinyooshea kidole serikali ya Beijing kwa kuiita “mwezeshaji madhubuti” wa Urusi katika vita vya Ukraine.

Katika taarifa yake fupi wizara ya ulinzi ya China imesema vikosi kutoka pande zote mbili vinashiriki doria katika Bahari ya Pasifiki ya magharibi na kaskazini na kwamba operesheni hiyo haina uhusiano wowote na hali ya sasa ya kimataifa au kulenga wahusika wengine.

China: mazoezi yanalengo la kustawisha usalama

Mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Iran, Russia na China kusini mwa Iran
Mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Iran, Russia na China kusini mwa IranPicha: Iranian Army Office/ZUMA/picture alliance

Awali Jumamosi televisheni ya umma ya China-CCTV ilisema mazoezi hayo ambyao yalianzia katika jimbo la Guangdong na kutegemewa kuendelea hadi katikati ya Julai, yana lengo la kuonesha uwezo wa jeshi la majini na kukabiliana na vitisho vya kiusalama, kulinda amani na utulivu duniani na kikanda.

Shirika hilo liliongeza kwa kusema luteka hiyo itajumuisha mazoezi ya kujikinga na makombora ya masafa marefu, mashambulizi ya baharini na ya anga.

Shirika la Habari la China Xinhua limearifu kuwa vikosi vya wanamaji vya China na Urusi vitafanya majairibio ya  kijeshi ya pamoja na mazoezi baada ya sherehe za ufunguzi katika mji wa Zhanjiang. Mazoezi haya ya pamoja yanafanyika baada ya mvutano wa hivi karibuni wa  katika ya China na washirika wa NATO wa juma lililopita.

Lawama za NATO kwa China dhidi ya Ukraine

Taarifa ya hitimisho yenye maneno makali, iliyoidhinishwa na wanachama 32 wa NATO katika mkutano wao wa kilele huko Washington, iliweka wazi kuwa China imekuwa na mwelekeo wa muungano wa kijeshi, ukisema wa “kiuwezeshaji madhubuti” katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Muungano huo, unazidi kuonesha wasiwasi wa kiusalama kutoka kwa Urusi na wafuwasi wake kwa upande wa bara la Asia. Na hasa China.

Katika kujibu taarifa ya NATO, China iliushutumu muungano huo kwa kutafuta usalama wake hata kwa kuwaathiri wengine  na kuuambia muungano huo usilete “machafuko” yale yale katika eneo la Asia. Wizara yake ya mambo ya nje ilisisitiza kuwa China ina msimamo wa haki juu ya vita kuhusu Ukraine.

Soma zaidi: China na Urusi zaendesha doria ya pamoja Bahari ya Pasifiki

Maafisa wa Marekani walisema juma lililopita katika doria yao ya kawaida walinzi wa maeneo ya pwani wa Marekani walikutana na meli kadhaa za kivita za China katika eneo la bahari la kimataifa lakini ndani ya ukanda wa kipekee wa kiuchumi wa Marekani,

Chanzo: AP

 

Related Posts