DAWASA YATANGAZA MAJI KUKOSEKANA KWA MUDA WA SAA 15 – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imewatangazia Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha Maji Ruvu Juu kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji siku ya Jumanne Julai 16,2024 kwa muda wa saa 15 kuanzia Saa 12 asubuhi hadi Saa 3 usiku.

Taarifa ya DAWASA iliyotolewa jana Julai 14, 2024 imeeleza kuwa sababu ni kuruhusu matengenezo kwenye bomba kuu la kusafirisha Maji ghafi kutoka Mtoni kwenda Mtamboni katika eneo la Mlandizi.

Maeneo yanayoathirika ni Ruvu darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mshikamano, Mbezi, Kimara, Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Msigani, Maramba Mawili, Tabata, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Ukonga, Pugu, Gongo la Mboto, Uwanja wa Ndege, Majumba sita, Kiwalani, Segerea, Kinyerezi na Kisarawe.

Related Posts