DJOCKOVIC APOTEZA KWA KINDA WA HISPANIA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Mchezaji bora wa muda wote wa mchezo wa tenisi duniani kwa upande wa wanaume Mserbia Novack Djockovic amepoteza mchezo wa fainali ya Wimbledon mbele ya kinda wa Hispania, Carlos Alcaraz.

Djockovic mwenye umri wa miaka 37 amekubali kichapo cha seti 3-0 za ushindi wa 6-2, 6-2 na 7-6 kutoka kwa Alcaraz mwenye umri wa miaka 21 ambaye ametumia muda wa chini ya saa mbili na nusu kumaliza ufalme wa Djokovic kwenye mashindano hayo ya Wimbledon.

Kwa ushindi huo Alcaraz anafanikiwa kuweka kabatini taji kubwa la nne lenye hadhi ya Grand Slam na kuzima ndoto ya Djockovic mwenye mataji saba ya Wimbledon kushinda taji lake la 25 la Grand Slam.

Related Posts