Mkazi wa Dar es Salaam ajishindia Gari kutoka Kampuni ya Kobe Motor ya Japan – MWANAHARAKATI MZALENDO

Siku ya tarehe 9 Julai mwaka 2024, itaendelea kuwa siku ya kumbukumbu kwa mkazi wa Dar es Salaam bwana Hafidh Amir Khamis baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa gari aina ya Nissan Note Rider Edition ya mwaka 2013 katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.

“Natoa shukrani zangu nyingi sana kwa kampuni ya Kobe Motor ya Japan. Ushindi huu mkubwa sikuutarajia hata kidogo lakini ni jambo lililonifurahisha sana na litaendelea kuwa la kihistoria kwangu,” alisema

“Nimekuwa nikifanya biashara na Kampuni ya Kobe Motor tangu mwaka 2022 na pia nimepata bahati ya kukutana na wafanyakazi wake kutoka Japana katika hafla ya chakula cha jioni ambapo pia niliweza kuifahamu kampuni hii zaidi,” aliongeza kusema muda mfupi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya gari aliloshinda.

Hafidh Amir Khamis alisema haikuwa rahisi kwake kuamini kuwa kweli ameshinda na aliipongeza Kampuni ya Kobe motor kwa zawadi hiyo ambayo inaonyesha kuwajali wateja wake.

Mkuu wa masoko wa Kobe motor Ken Aoki alisema zawadi hiyo imetolewa ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kutambua mchango wa wateja wake katika kusaidia kukua kwa kampuni hiyo na kuwa moja kati ya makampuni makubwa ya kuuza magari Tanzania na duniani kwa ujumla

“Tunayo furaha kubwa kukabidhi mfano wa hundi ya gari kwa mshindi wetu bwana Hafidh Amir Khamis. Gari bado lipo Japana, litashafirishwa kuja Tanzania na ndani ya kipindi cha mwezi mmoja atapokea gari lake,” alisema

Katika hatua nyingine Kampuni ya Kobe Motor imezindua utaratibu wa wateja kulipa 35% ya thamani ya gari na kupewa gari la ndoto yao huku kiasi kilichobaki kikilipwa kwa kipindi cha miezi 12 au 24.

No alt text provided for this imageThabit Adam (wa tatu kushoto) akimwakilisha Hafidh Amir Khamis, mshindi wa gari katika bahati nasibu iliyochecheshwa na kampuni ya Kobe motor akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Kobe Motor muda mfupi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi wa gari aliloshinda katka hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo Mikocheni jijini Dar es Salaam.No alt text provided for this imageMkuu wa masoko wa kampuni ya kuuza magari yaliyotumika kutoka Japan Kobe Motor Ken Aoki (kulia) akimpongeza Thabit Adam ambaye alimwakilisha mshindi wa gari (2024 free car lottery winner) kutoka Kobe motor Hafidh Amir Khamis muda mfupi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya gari katika hafla iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo Mikochen jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.No alt text provided for this image Afisa Mauzo mwandimizi wa kanda ya Afrika wa kampuni ya kuuza magari yalitumika kutoka Japan ya Kobe Motor Muhammed Fahmi (kulia) akimpongeza Thabit Adam ambaye alimwakilisha mshindi wa gari (2024 free car lottery winner) kutoka Kobe motor Hafidh Amir Khamis muda mfupi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya gari katika hafla iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo Mikochen jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.No alt text provided for this imageAfisa Mauzo mwandimizi wa kanda ya Afrika wa kampuni ya kuuza magari yalitumika kutoka Japan ya Kobe Motor Muhammed Fahmi (kulia) akimpongeza Thabit Adam ambaye alimwakilisha mshindi wa gari (2024 free car lottery winner) kutoka Kobe motor Hafidh Amir Khamis muda mfupi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya gari katika hafla iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo Mikochen jijini Dar es Salaam mwishoni mwawiki. Kushoto ni Mkuu wa masoko wa kampuni ya kuuza magari yaliyotumika kutoka Japan Kobe Motor Ken Aoki (kulia)

#KonceptTvUpdates

 

Related Posts