Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameendelea na ziara ya Kiserikali ya Kata kwa Kata katika jimbo la Songea Mjini akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Katika ziara hiyo Mhe. Ndumbaro ameambatana na wataalam mbalimbali kutoka sekta ya elimu, afya, miundombinu na nishati ambao ili kutoa ufafanuzi na majibu ya hoja mbalimbali za wananchi.
Ziara hiyo inaendelea tena leo Julai 15, 2024 katika kata nyingine tatu za jimbo hilo.