RAIS SAMIA AZINDUA HOSPITALI YA WILAYA YA NKASI – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Rais Samia Suluhu Hassan leo Julai 15, 2024 ameanza ziara mkoani Rukwa ambapo amezindua Hospitali ya Wilaya ya Nkasi yenye majengo na miundombinu ya kisasa iliyopo Namanyere mkoani humo.

 

Hospitali hiyo hadi kukamilika kwake imegharimu zaidi ya shilingi bilioni 5 na sasa inatoa huduma bora zaidi kwa wananchi wa wilaya hiyo.

 

Rais Samia amewataka wahudumu wa afya katika hospitali hiyo kuendelea na moyo wa kuwahudumia wagonjwa bila kinyongo akitolea mfano wa mtoto aliyezama kwenye maji na kupatiwa matibabu ya haraka katika hospitali hiyo ambapo sasa anaendelea vizuri.

 

Amesema hilo pia liliwezekama kutokana na hospitali hiyo kuwa na vifaa vya kisasa.

 

HABARI PICHA

Related Posts