Trump asimulia alivyookolewa, asema alipoteza viatu

New York. Mgombea urais wa Chama cha Republican, Donald Trump saa chache tangu ashambuliwe kwa risasi akiwa anahutubia, amesimulia namna alivyopoteza viatu wakati akiokolewa.

Tovuti ya CNN imeripoti kuwa viatu hivyo vilipotea wakati anatolewa jukwaani na maofisa wa ‘Secret Service’

Trump ambaye ni Rais wa zamani wa Taifa hilo, alishambuliwa akiwa anahutubia Jumamosi Julai 13, 2024 kwenye mkutano, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni zake kabla ya uchaguzi mkuu wa taifa hilo.

CNN imeandikwa kuwa sauti ya Trimp ilisikika akiwaomba maofisa hao kumpa nafasi avae viatu vyake akiwa anaondoka jukwaani baada ya shambulio hilo.

“Ngoja nichukue viatu vyangu. Acha nichukue viatu vyangu,” alisema Trump.

“Nimekupata mkuu. Nimekuelewa mkuu,” alijibu ofisa mmoja.

Akifanya mahojiano na gazeti la New York Post, Trump alisema; “Wakati wa purukushani ya kuniokoa, viatu vyangu vilinivuka. Nawashukuru sana maofisa wa ulinzi wa siku ile ya Jumamosi,” amesema.

Related Posts