Durant kumpa namba Tatum | Mwanaspoti

KATIKA hiyo timu ya Taifa ya Marekani ya mchezo wa kikapu (Team USA) kuna shughuli pevu ya wachezaji unaambiwa, kuelekea michuano ya Olimpiki nchini Ufaransa ambapo imejaa mastaa unaowajua wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA).

Kuanzia LeBron James, Steph Curry, Jayson Tatum, Anthony Edwards, Anthony Davis, Kevin Durant, Jrue Holiday na Joel Embiid ambao ndani yao kila mmoja anaweza kuanza kikosi cha kwanza (starters) wakimpa kazi kubwa Kocha Steve Kerr.

Wakati timu hiyo ikiwa Las Vegas kwa mechi za maandalizi, Jrue Holiday na Jayson Tatum wamekuwa mbadala wa Kevin Durant ambaye hajawa fiti baada ya kuumia na kama ataendelea kutokuwa fiti atampa nafasi Tatum kuanza kwenye nafasi yake licha ya staa huyo bingwa wa NBA mwaka huu kuwa tayari kucheza kutokea benchi (sixth man) katika kikosi hicho kinachokwenda kusaka taji la Olimpiki dhidi ya mataifa mengine.

Related Posts