ISHU YA LAMECK LAWI IPO HIVI, SIMBA NA COASTAL WAVUTANA SHATI – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Said Soud ametolewa nje baada ya mwanasheria upande wa Simba SC kuomba Mwenyekiti huyo atolewe nje.

 

 

Said Soud ametolewa nje kwenye shauri la kesi la mchezaji Lameck Lawi baada ya Mwenyekiti huyo kutajwa kuwa ni mwanachama na shabiki wa Coaster Union.

 

 

Said Soud ametoka nje amewaachia wajumbe waendelee na shauri hilo linalosikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwenye ofisi za TFF, zilizopo Ilala Dar es Salaam.

 

 

Coastal Union na Simba zimeingia kwenye mgogoro wa kumgombania beki Lameck Lawi Simba ikimtangaza kama mchezaji wao na Coastal ikisema mchezaji huyo hajauzwa bado ni mali ya Coastal.

 

 

Klabu ya Coastal Union yenye maskani yao mkoani Tanga ina viongozi mbalimbali na wanachama (TFF).

◉ Wallace Karia ›› Mwanachama Coastal.
◉ Steven Mguto ›› Mwenyekiti Coastal.
◉ Said Soud ›› Mwanachama Coastal.

 

Kilichotokea ni kwamba Wagosi wa Kaya walidai kwamba Simba wameshindwa kufuata makubaliano ya kimkataba ambapo pesa za usajili wa Lameck Lawi zilitakiwa kuingizwa zotekabla ya May 30.

 

Simba walihitaji wamlipe Million 5 kwa Kila mwezi kama mshahara wake wa mkataba, baada ya Simba kuchelewa kufanya malipo ya uhamisho wa mchezaji huyo kutoka Coastal Union ambayo yalipaswa kufanyika tarehe 31/06/2024, imetokea timu Moja nyingine kutoka nchini Ubelgiji ambayo inahitaji kumlipa mchezaji Lameck Lawi kwa mwezi Tshs 25 M

 

Baada ya Coastal Union kuona mzigo wa maana wamebadili uelekea na kuamua kurejesha fedha ambazo Simba waliweka kwenye Account nusu ya makubaliano Tshs 100 M badala ya Million 200,000,05 ambazo zilipaswa kuwekwa kwenye Account ya Coastal Union tarehe 31 Jun 2024.

 

Mpaka sasa Lameck Lawi ameandika Barua kuomba yale makubaliano ya awali na Simba sc yavunjwe.

 

Upande wa Simba iliwakilishwa na mwanasheria wake mkuu Hosea Chamba ,hakuna maamzi yaliyofanyika kuamua hatima ya mchezaji Lameck Lawi kesi imeahirishwa mpaka wakati mwingine kamati itakapoketi tena

 

 

Lameck Lawi sio miongoni mwa wachezaji wa Simba waliopo kambini Misri, alibakia Dar katika klabu ya Coastal Union lakini pia hajacheza mechi hata moja ya mashindano  ya KAGAME CUP.

 

Chanzo : Soka la Bongo 

Related Posts