Makambo apewa mmoja Coastal Union

COASTAL Union imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Mashujaa, Athuman Masumbuko ‘Makambo’ kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mshambuliaji huyo msimu wa 2023 aliibuka na tuzo ya mfungaji bora wa mashindano ya Ligi ya Vijana chini ya miaka 20 akiweka kambani mabao saba, Mtibwa Sugar ilipoibuka mabingwa.

Awali, Geita Gold iliyoshuka daraja msimu uliopita ilikuwa ya kwanza kupata saini ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Mtibwa U-20.

Akizungumza na Mwanaspoti, kiongozi mmoja wa Coastal ambaye hakutajwa jina lake litajwe, amesema wamempa mkataba wa mwaka mmoja kinda huyo.

“Ni kweli tumekubaliana na kesho atakuja Tanga kwa ajili ya kusaini nyaraka hizo, ni mchezaji mzuri ambaye kwa kiwango alichoonesha tunaamini anaweza kutusaidia,” amesema kiongozi.

Related Posts