MBUNGE ZUENA BUSHIRI AWASHA MOTO MWANGA..

NA WILLIUM PAUL, MWANGA.

MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri ameendelea na ziara yake wilayani Mwanga ambapo amekabidhi mashuka yaliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kituo cha Afya cha Mwanga.

Akikabidhi mashuka hayo, Zuena alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imeendelea kupambana kuhakikisha changamoto zinazoikabili sekta ya Afya zinapatiwa ufumbuzi ambapo imewekeza katika miundombinu ya Afya pamoja na upatikanaji wa Dawa.

Alisema kuwa, katika kuwajali wananchi wake, Rais ametoa mashuka ambapo kwa niaba yake ameyakabidhi na kuwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali yao pamoja na kulinda miundombinu hiyo inayoletwa.

“Rais Dkt. Samia anatambua changamoto ambazo zinaikabili sekta ya Afya na amekuwa akipambana kuhakikisha anazimaliza na kwa kutambua umuhimu wa wananchi wake ametuma nije kukabidhi mashuka haya haya kituo cha Afya Mwanga” Alisema Zuena.

Mara baada ya kukabidhi mashuka hayo, Mbunge huyo alifanya mkutano wa hadhara wa wananchi kuwakumbusha umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu.

Aliwataka kutumia fursa hiyo kuwachagua viongozi bora watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ambapo alisema kuwa viongozi wazuri wanatokana na Chama cha Mapinduzi.

Katika mkutano huo, wapo wananchi walioonyesha kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo waliamua kujiunga na Jumuiya ya Wanawaka wa Chama cha Mapinduzi (UWT) ambapo Mbunge Zuena aliwapokea na kuwakabidhi kadi za uanachama. 


Related Posts