MRADI WA AFYA KWA VIJANA YAWAKOMBOA VIJANA WA FULWE MOROGORO

MRADI wa Afya kwa Vijana unaodhaminiwa na Umoja wa Ulaya umefanikiwa kuwatoa gizani vijana wanaoishi katika kijiji cha Fulwe kata ya Mikese mkoani Morogoro baada ta kuwapatia elimu ya afya ya uzazi.

Mradi huo unaodaminiwa na umoja wa Ulaya na kutekelezwa na mashirika matatu ; Marie Stopes Tanzania kwa kushirikiana na SIKIKA na DSW ulitoa mafunzo ya Afya ya Uzazi kwa watoa huduma wa ngazi ya jamii, vijana vinara na watoa huduma za afya katika zahanati ya kijiji hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoa huduma hao wamesema kuwa vijana ni kundi linalotakiwa kupewa elimu ya afya ya uzazi ili kuokoa kizazi kijacho.

Mtoa huduma kwa vijana wa rika barehe Rukia ramadhani Mwamba alisema kuwa kuna kundi kubwa la vijana wanaopata magonjwa ya ngono kutokana na kundi hilo kutokua na elimu ya kutosha.

Alisema kupitia mradi huo katika kijiji cha fulwe vijana wamekuwa wakipata elimu hiyo ambayo imewasaidia kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake mzee Nurdin Said alisema kuwa alifanyakazi kubwa ya ushawishi kwa vijana hao kuwasikiliza watoa huduma baada kuona ipo haja ya vijana kupatiwa elimu ya afya ya uzazi ili kupunguza mimba za utotoni ambazo zinapelekea wingi wa watoto wa mtaani.

“Mimi nilikuwa napita tu bahati nzuri wanaosimamia mafunzo haya mimi wananifahamu na wakajua mimi nipo vizuri kuongea na wazee na vijana wakanambia natakiwa kuongea na vijana kuhusu elimu ya uzazi na mimi nikaona ipo haja ya vijana kupata elimu hii ili waendane na elimu ya sasa hivi”alisema Nurdin.

Aidha mzee Nurdin alitoa ushauri kwa watoa huduma kutokana na vijana kutopata muda wa kusikiliza madarasa haya basi wajitahidi kufika katika maeneo ambayo vijana wapo kama vile kwenye viwanja vya mpira.




Related Posts